1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan: Nani anaruhusiwa kwenda Ujerumani?

Hawa Bihoga
15 Agosti 2023

Ujumbe wa kimataifa nchini Afghanistan, ulioanza mwaka 2001 kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, uliporomoka Agosti 15, 2021.

USA I Aussenministerin Baerbock in New York - ICC
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Wafanyakazi wa Kiafghan waliovisaidia vikosi vya Ujerumani walikimbia haraka kuitoroka nchi yao, na wengi bado wanasubiri msaada. 

Chini ya mazingira ya vurugu vikosi vya jeshi la Ujerumani viliwaondoa Wajerumani na wa Afghan waliotoa ushirikianokwa miaka mingi katika hadhi za kijeshi na kiraia. Lakini wenyeji wengi hawakuweza kuokolewa mara moja. Katika tangazo la serikali, kansela wa wakati huo Angela Merkel aliahidi kusaidia.

Hata hivyo miaka miwili baada ya ahadi hii, maelfu ya wafanyakazi wa Kiafghani, familia zao na watu wengine walioko hatarani, bado wanasubiri kuja nchini Ujerumani. Sambamba na idara za serikali, mashirika kadhaa ya kiraia pia yanawaangalia waafghani walioko hatarini.

Soma pia:Agosti 15 ni miaka miwili tangu Taliban irejee madarakani Afghanistan

Waziri wa mambo ya ndani  Nancy Faeser, aliiambia kamati ya haki ta binadamu ya bunge la Ujerumani mnamo Juni, kwamba  Ujerumani imewachukuwa wafanyakazi wa zamani wa msaada takribani 20,000 pamoja na familia zao tangu Januari 2022.

Watu hao walikuwa kwa sehemu kubwa wanalifanyia kazi jeshi la Bundeswehrna katika sekta ya ushirikiano wa kimaendeleo.

Ushuhuda kutoka kwa mashahidi katika kamati ya uchunguzi ya bunge juu ya Afghanistan, unaonyesha kuwa Ujerumani bado inaendelea kukumbana na matatizo katika kuwasaidia wafanyakazi wa zamani wa Kiafghan.

Kamati hiyo pia iantaka kubaini kwanini hakukuonekana kuwa na mpango stahiki wa kuokoa wafanyakazi wa ndani wakati Taliban ilipochukuwa madaraka.

Ujerumani yakiri kutojiandaa vya kutosha

Wizara ya shirikisho ya Ujerumani inayoshughulikia ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, BMZ, ilikiri kwamba wizara yao haikuwa imejiandaa vya kutosha kwa hali hiyo.

Wazo la kuwahifadhi wafanyakazi wa ndani waliokimbia katika mataifa jirani kama vile Tajikistan, Uzbekistan au Pakistan, lilizimgatiwa pia lakini hakuna kati ya serikali hizo ilikuwa tayari kuchukuwa wakimbizi kutoka Afghanistan.

Wanawake wa Afghanistan waelezea maisha yao kupitia uchoraji

02:56

This browser does not support the video element.

Tangu kuingia madarakani kwa Taliban, BMZ pekee imeahidi kuchukuwa karibu wafanyakazi 15,000 wa zamani wa mpango wa ushirikiano wa maendeleo wa Ujerumani pamoja na familia zao.

Kati yao, karibu 11,600 walikuwa wamesafiri hadi Ujeurmani kufikia mwanzoni mwa Julai mwaka huu, msemaji wa wizara hiyo aliiambia DW.

Soma pia:Kiongozi wa juu Afghanistan aonya dhidi ya mashambulizi nje ya nchi

Kwa wanaosalia 3,400, takribani 600 kati yao wako njiani kupitia nchi jirani. MBZ kwa msaada wa taasisi ya Ujerumani kwa ajili ya ushikirikiano wa kimataifa, GIZ, inawasaidia wafanyakazi wa zamani kwenyemichakato yao ya kuhamia Ujerumani, pamoja na huduma zao na makazi katika mataifa wanakopitia.

Wakati huo huo, Taliban wanazidi kudhibiti haki za binadamu, hasa kwa wanawake na wasichana. Ndiyo maana serikali ya Ujerumani ilianzisha mpango wa ziada wa msaada, ulioanzishwa na waziri wa mambo ya nje, Annalena Baerbock.

Ingawa maelfu ya Wafghani waliohudumu kama wafanyakazi wa msaada wamekimbilia Ujerumani, Ujerumani inaendelea kutoa msaada wa kibinadamu. Hata hivyo BMZ imesema haijaajiri wafanyakazi wengine wa ndani tangu Taliban iliporejea madarakani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW