1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Afghanistan: Wanawake waandamana kupinga marufuku dhidi yao

26 Machi 2023

Zaidi ya wanawake kumi na wawili wameandamana magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan Kabul kupinga hatua ya watawala wa Taliban kuwapiga marufuku dhidi ya kusoma sekondari na vyuo vikuu.

Afghanistan Frauen demonstrieren für das Recht auf Bildung in Kabul
Picha: AFP

Watawala wa Taliban walitangaza marufuku dhidi ya wanawake na wasichana kupata elimu ya sekondari na vyuo vikuu.

Wanawake hao waliandamana huku wakiimba "elimu ni haki yetu."

Vituo kadhaa vya habari nchini Afghanistan vimeripoti kuwa vikosi vya Taliban viliingilia kati na kuwatawanya waandamanaji.

Video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimeonyesha wasichana kadhaa wakizozana na vikosi vya Taliban huku wakitetea harakati za wanawake kupata elimu.

Kundi la Taliban lilirejea madarakani baada ya kuondoka vikosi vya NATO nchini Afghanistan mnamo Agosti, 2021. Wanamgambo hao walirejesha tena sheria na kanuni kali licha ya wito wa Jumuiya ya Kimataifa.