SiasaAsia
Afghanistan yaapa kulipiza kisasi dhidi ya Pakistan
18 Machi 2026
Matangazo
Wakati wa mazishi ya baadhi ya waliouawa mjini Kabul, Haqqani amesema watalipiza kisasi na akawataja waliohusika katika shambulizi hilo la Jumatatu usiku kuwa ''wahalifu.''
Mamlaka ya Taliban imesema takriban watu 400 waliuawa na zaidi ya 200 kujeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo ndilo baya zaidi kutokea katika mgogoro wa sasa kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Hata hivyo Pakistan imekanusha madai ya serikali ya Taliban kwamba kituo hicho kililengwa kwa makusudi na kusema kililenga kushambulia kambi za kijeshi na miundombinu ya msaada kwa magaidi.