Afghanistan yadai Pakistan imeishambulia na kuuwa raia wake
22 Februari 2026
Pakistan imesema wanamgambo hao wanaishambulia nchi hiyo kutoka Kabul.
Utawala wa Taliban umesema wanawake na watoto ni miongoni mwa watu 18 waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa katika shambulizi la Jana Jumamosi. Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema inapanga shambulio la kulipiza kisasi, hali ambayo inahofiwa kuzidi kutia doa mahusiano ya mataifa hayo mawili.
Shambulizi hili limetokea siku kadhaa baada ya Afghanistan kuwaachia huru wanajeshi watatu wa Pakistan katika juhudi zilizosimamiwa na Saudi Arabia kwa nia ya kupoza mvutano kati ya pande hizo mbili kufuatia miezi kadhaa ya makabiliano makali ya mpakani.
Pakistan inaituhumu Afghanistan kutoa hifadhi kwa makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa mipaka yake madai ambayo watawala wa Taliban wamekuwa wakiyakanusha.