1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia: Afisa mwandamizi wa chama cha upinzani akamatwa

Angela Mdungu
14 Julai 2024

Katibu Mkuu wa chama cha upinzani chenye itikadi kali za kiislamu nchini Tunisia cha Ennahdha, Ajami Lourimi amekamatwa jana Jumamosi.

Mkuu wa chama cha Ennahdha Rached Ghannouchi
Mkuu wa chama cha Ennahdha Rached Ghannouchi amekuwa gerezani tangu Aprili mwaka 2023Picha: Hasan Mrad/DeFodi Images/picture alliance

 Taarifa ya kukamatwa kwake imetolewa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Taarifa hiyo imeeleza kwamba, Lourimi, alikamatwa bila ruhusa ya mahakama pamoja na wenzake wawili katika mji wa Borj Al Amrim, ulio karibu kilomita 37 kutoka mji mkuu Tunis.

Hata hivyo chama hicho ambacho Mkuu wake Rached Ghannouchi amekuwa gerezani tangu Aprili mwaka jana, hakikutoa sababu yoyote ya kukamatwa kwa Lourimi.

Mwezi Septemba mwaka uliopita, viongozi wawili wa Ennahdha yaani Waziri Mkuu wa zamani Hamadi Jebali na Mondher Ouniss aliyekuwa kaimu mkuu wa chama hicho tangu Ghannouchi alipokamatwa, nao walitiwa mbaroni. Serikali ya Rais  Kais Saied ilizifunga ofisi za chama hicho baada ya Ghannouchi kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na ugaidi.