1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa mwandamizi wa China afanya ziara huko Pyongyang

Sylvia Mwehozi
13 Aprili 2024

Afisa wa ngazi ya juu wa China Zhao Leji amesema Beijing ina sera ya kimkakati ya kuitetea na kuendeleza uhusiano wa karibu na Korea Kaskazini.

China | Zhao Leji
Afisa wa ngazi ya juu wa China Zhao LejiPicha: Ng Han Guan/AP Photo/picture alliance

Afisa wa ngazi ya juu wa China Zhao Leji amesema Beijing ina sera ya kimkakati ya kuitetea na kuendeleza uhusiano wa karibu na Korea Kaskazini.

Leji, ambaye ni mwenyekiti wa Bunge la China na anayezingatiwa kuwa kiongozi wa tatu kwa ukubwa wa madaraka ndani ya chama tawala cha kikomunisti, aliwasili Pyongyang siku ya Alhamis.

Afisa huyo amekutana na mwenzake wa Pyongyang Choe Ryong Hae na kujadili nia ya kutanua mahusiano na kubadilishana uzoefu kwenye uga wa siasa, uchumi na utamaduni.

Duru zinasema mazungumzo hayo ndiyo ya ngazi ya juu zaidi kati ya viongozi wa pande hizo mbili ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita. Pyongyang imekuwa ikijaribu kuboresha ukaribu wake na China pamoja na Urusi chini ya kiwingu cha kutengwa kimataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW