1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Afisa wa polisi awaua watu wanne katika sinagogi, Tunisia

10 Mei 2023

Afisa wa polisi nchini Tunisia amewauwa watu wanne katika sinagogi kongwe zaidi barani Afrika, katika shambulio la jana Jumanne lililoibua hamaki wakati wa hijja ya kila mwaka ya Mayahudi kwenye kisiwa cha Djerba.

Shambulizi kwenye sinagogi nchini Tunisia limeibua mashaka ya usalama kwa mahujaji
Baadhi ya waumini huwa wanakwenda kwenye sinagogi hili kuhijiPicha: Jihed Abidellaoui/REUTERS

Wizara ya mambo ya ndani imesema askari huyo aliwapiga risasi wageni wawili, akiwemo raia wa Ufaransa, na askari wenzake wawili, kabla ya yeye mwenyewe kupigwa risasi na kuuawa. Wageni wengine wanne na maafisa wa watato wa polisi walijeruhiwa katika shambulio hilo, la kwanza dhidi ya wageni kutoka nje nchini Tunisia tangu 2015, na la kwanza dhidi ya mahujjaji wa Sinagogi la Ghriba tangu shambulio la kujitoa muhanga lililoua watu 21 mwaka 2002. Wizara ya mambo ya nje ya Tunisia iliwatambua wageni wawili waliouawa kuwa ni raia wa Tunisia mwenye umri wa miaka 30 na raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 42, lakini haikutoa majina yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW