1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Afisa wa Umoja wa Mataifa ahimiza mapigano yasitishwe Gaza

Josephat Charo
30 Oktoba 2024

Afisa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa kusitisha haraka mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuitisha suluhisho la mataifa mawili

Marekani New York | Mratibu Maalum wa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati | Lango la Wennesland
Tor Wennesland, Mratibu Maalum wa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.Picha: Lev Radin/Sipa USA/picture alliance

Afisa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa kusitisha haraka mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuitisha suluhisho la mataifa mawili, huku akionya kwamba hali katika Mashariki ya Kati ni hatari zaidi kuliko ilivyokuwa katika miongo iliyopita.

Katika kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati na suala la Wapalestina, Tor Wennesland, mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, alisema eneo hilo liko katika hali ya hatari isiyomithilika.

Soma pia: Misri yapendekeza kusitishwa mapigano kwa siku mbili Gaza

Alisema ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa, haitawezekana kimsingi kuibadili hali inayoendelea sasa katika Ukanda wa Gaza.

Riyad Mansour, muangalizi maalumu wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina katika Umoja wa Mataifa alisema vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza vimewatumukiza  Wapalestina wengi waliopoteza majakzi katika hali ya kukata tamaa, huku umma mzima wa kaskazini mwa Gaza ukikabiliwa na kitisho cha kifo. Aliikosoa Israel kwa kutoheshimu sheria z akimataifa na kwa kuvunja sheria za Umoja wa Mataifa.