1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

UN yatahadharisha kuhusu hali mbaya nchini Haiti

23 Oktoba 2024

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha hii leo kuwa ghasia za magenge ya wahalifu zinaongezeka nchini Haiti.

Polisi wa Haiti wakikabiliana na magenge ya wahalifu
Polisi wa Haiti wakikabiliana na magenge ya wahalifuPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Afisa huyo amesema ghasia hizo zinaongezeka nchini Haiti, licha ya kutumwa kwa kikosi cha kimataifa kusaidia polisi wa nchi hiyo ya Caribbean.

Maria Isabel Salvador, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali ya usalama bado ni tete nchini Haiti, huku kukiwa na ongezeko la ghasia za hali ya juu.

Soma pia: Baraza la Usalama la UN laongeza vikwazo vya silaha Haiti

Kauli ya Bi Salvador imetolewa wiki chache tu baada ya raia 115 kuuawa na makumi ya wengine wakijeruhiwa katika shambulio la wahalifu katika mji wa kati wa Port Sonde, tukio ambalo amesema liligubikwa na ukatili wa kupindukia.

Afisa huyo ameendelea kusema kuwa Haiti kwa sasa ina wakimbizi wa ndani wapatao 700,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, na kwamba hali ya kibinadamu ni mbaya zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW