1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Afisa wa zamani akiri kuhusika mauaji ya rais wa Haiti

6 Desemba 2023

Afisa wa zamani aliyeshirikiana na Mamlaka ya kudhibiti Dawa za kulevya nchini Marekani (DEA), amekuwa mtu wa nne kukiri jukumu lake la kuhusika katika mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moise mnamo mwaka 2021.

Haiti I Foto des der verstorbenen haitianischen Präsidenten Jovenel Moise während seiner Gedenkfeier
Muombolezaji akiwa na picha ya rais wa zamani wa Haiti, Jovenel Moise, wakati wa mazishi yake Januari 2022.Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Joseph Vincent mwenye uraia pacha wa Marekani na Haiti, ambaye pia alikuwa mtoa taarifa kwa mamlaka ya DEA alikuwa miongoni mwa washtakiwa 
11 wakiwemo wanajeshi wa zamani wa Colombia na wafanyabiashara.

Soma zaidi: Mshukiwa mkuu wa mauaji ya rais wa Haiti akamatwa

Watu hao wanashtumiwa kusaidia usambazaji wa fedha na silaha pamoja na  kutekeleza shambulio la usiku katika makaazi ya Rais Jovenel katika mji mkuu Port-au-Prince, mauaji ambayo yaliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo wa kiutawala na kiusalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW