1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Angela Mdungu
2 Agosti 2019

Kati ya yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani kuhusu Afrika, ni pamoja na kutolewa kwa hukumu ya kesi ya wachimbaji madini nchini Afrika a Kusini.

Afrika Mine
Picha: Issouf Sanogo/Getty Images

Mhariri wa die tageszeitung ameiita hukumu hiyo kuwa ni hukumu iliyocheleweshwa. Gazeti hilo limeandika kuwa mahakama kuu nchini Afrika ya kusini imepitisha makubaliano yanayotaka kulipwa fidia wachimbaji hao, kutokana na maradhi ya kifua kikuu na maradhi mengine ya mapafu yanayotokana na vumbi katika migodi ya dhahabu, na kwamba wengi wa wachimbaji hao tayari wamekufa.

Wachimbaji hao, wameifanya dhahabu ya Afrika ya Kusini kuonekana huku afya zao zikiharibika. Lakini sasa uamuzi wa kihistoria wa mahakama umeamua walipwe fidia. Ni baada ya miaka 15 ya migogogro ya kisheria, maelfu ya wafungwa wanasherehekea ushindi wao  dhidi ya kampuni sita za za uchimbaji madini nchini humo.

 Zaidi die tageszeitung limeandika kuwa makampuni hayo ya kimataifa  yametakiwa kufanya malipo ya randi bilioni 5 sawa na Euro milioni 315 katika mfuko maalumu ambao utazifikisha fedha hizo kwa waathiriwa na familia zao, na iwapo fedha hizo hazitatosha, makampuni hayo yatatakiwa kulipa fedha zaidi.

Nalo Gazeti la Neue Zürcher limeandika juu ya shambulio lililofanywa na kundi la Boko Haramna kuua watu zaidi ya 60 nchini Nigeria. Gazeti hili limeandika, kwa  miaka 10 sasa kundi la kigaidi la Boko haramu limekuwa likilitesa eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria nakuliacha jeshi la nchi hiyo lisijuenini la kufanya. Jumamosi iliopita zaidi ya watu sitini waliuawa katika shambulio wakati wa maziko nchini Nigeria.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji kilicho karibu na mji wa Maiduguri kwenye jimbo la Borno. Shambulizi hilo ni kubwa zaidi kutokea kwa mwaka huu nchini humo. Gazeti hilo limeandika kuwa kundi hilo lenye itikadi kali la Boko Haram limesema shambulizi hilo ni la kujibu mapigo baada ya wanakijiji hao kujilinda dhidi yao wiki mbili zilizopita.

Zaidi gazeti la Neue Zücher limeandika tayari ni miaka kumi sasa, tangu kundi hilo la Boko Haram lijibadilishe toka kuwa kundi la kiislamu na kuwa taasisi ya kigaidi na kwamba kuuawa kwa mwanzilishi wa kundi hilo Mohammed Yusuf ilikuwa kama kichocheo cha mashambulizi yanayoendelea baada ya mtangulizi wake, Aboubakar Shekau kuwataka wafuasi wa kundi hilo kuanzisha vita takatifu.

Tangu wakati huo, kundi la Boko Haram limeshaua takribani watu 27,000 huku wengine milioni 2.5 wakilazimika kuyakimbia makazi yao. Gazeti hilo liliendelea kuandika kuwa Baada ya kuchaguliwa kwa Jenerali wa zamani wa jeshi Muhammadu Buharu kuwa Rais wa Nigeria mwaka 2015, shinikizo la jeshi kwa kundi hilo liliongezeka, huku jeshi hilo likiungana na majeshi ya Chad.

Blätter für deutsche und internationale Politik limeandika juu ya mlipuko wa homa ya Ebola ambayo habari zake zimekuwa zikitikisa vyombo vya habari duniani kwa majuma kadhaa sasa. Gazeti hilo limeandika, Kwa mwezi uliopita pekee, takribani watu laki tatu walilikimbia eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo bila ya Jumuiya ya kimataifa kufahamu. Wengi wao wanabaki kuwa watu wasio na makazi ndani ya Kongo lakini zaidi ya 29,000 wamekimbilia nchi jirani ya Uganda  tangu mwanzo wa mwaka huu, na kinachowasukuma kufanya hivyo ni hofu mara mbili: hofu ya vita-na hofu ya homa ya ebola.

Gazeti hili limeandika kuwa mlipuko wa mwisho wa ugonjwa huu wa kuambukiza ulitokea miaka michache tu iliyopita: kati ya mwaka 2014 na 2016, Ebola iliua zaidi ya watu 1,300  Magharibi mwa Afrika pekee. Hii haikuwa kutokana na mfumo mbaya wa afya pekee wa nchi zilizoathiriwa bali shirika la Afya duniani lililifumbia macho tatizo hilo la kuwa mtazamaji kwa kupindi kirefu, lakini iwapo kuna mtu anadhani kuwa WHO ilijifunza kutokana na janga hilo na kwamba litachukua hatua za haraka Kongo, mtu huyo atakuwa amekosea.

Vyanzo: Deutsche Zeitungen

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW