Afrika Kusini imeanza wiki ya maombolezo
27 Desemba 2021Matangazo
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemtaja Tutu kuwa mtu aliyekuwa na uadilifu wa kipekee na mwanaharakati thabiti dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama pia amemtaja Tutu kuwa kielelezo bora cha maadili.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Tutu alikihamasisha kizazi cha viongozi wa Afrika ambao walizingatia mbinu zake zisizo za vurugu katika mapambano ya uhuru.
Viongozi wa Ulaya pia wametoa rambirambi zao, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amemtaja Tutu kuwa kiungo muhimu katika harakati za kujenga Afrika Kusini mpya na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema mapambano huyo dhidi ya ubaguzi wa rangi na mchango wake katika kulinda haki za binadamu, vitaenziwa daima.