Timu nyengine 3 za Afrika zafuzu kushiriki Kombe la Dunia
15 Oktoba 2025
Matangazo
Timu hizi tatu zinajiunga na Algeria, Cape Verde, Misri, Morocco, Senegal na Tunisia katika mashindano hayo yatakayoandaliwa nchini Marekani, Canada na Mexico.
Timu za Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon na Nigeria zimeyaweka hai matumaini yao ya kujaza nafasi ya kumi kwa bara la Afrika na zitacheza mechi moja moja za nusu fainali na fainali itakayochezwa nchini Morocco mwezi ujao wa Novemba na washindi watafuzu kwa michuano hiyo yakombe la dunia mwaka 2026.