Afrika kusini yakabidhiwa usukani wa kuandaa michuano ya kombe la dunia 2010
8 Julai 2006Na hatimae Berlin ambako Afrika kusini imejitembeza ikiwa kama mwenyeji wa michuano ijayo ya fainali za kombe la dunia.Mwaka 2010 bara zima la Afrika litadhihirisha linajiamaini,sawa na ilivyoshuhudiwa mwaka 1954,Ujerumani ilipoibuka na ushindi baada ya vita,amesema rais Thabo Mbeki alipokua akionyesha nembo ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2010.Afrikia kusini itatekeleza ahadi ilizptoa na kuandaa kwa ufanisi michuano hiyo-amesisitiza rais Thabo Mbeki.Mwenyekiti wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA,Joseph Blatter ameelezea matumaini kuona fainali za kombe la dunia zitachangia kumaliza mizozo ya kijamii nchini Afrika kusini.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema wakati wa sherehe hizo,hata kama Ujerumani haitocheza fainali,imeshinda lakini kwasababu imeandaa “ michuano bora kabisa ya kombe la dunia kuwahi kushuhudiwa.” Ujerumani inateremka uwanjani baadae hii leo kuania nafasi ya tatu dhidi ya Ureno.