1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini na madai ya Marekani kuiuzia Urusi silaha

13 Mei 2023

Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imemuita balozi wa Marekani kupinga madai yake kwamba nchi hiyo imeiuzia Urusi silaha.

South Africa Arms To Russia I The Russian vessel Lady R
Picha: AP/picture alliance

Siku ya Alhamisi, Balozi Reuben Brigety alidai kuwa silaha zilipakiwa kwenye meli ya Urusi iliyotia nanga katika eneo la kikosi cha jeshi la majini cha Afrika Kusini cha Simonstown mwezi Desemba.

Afrika Kusini imesema haina rekodi ya kuidhinisha mauzo ya silaha na Rais Cyril Ramphosa ameamuru uchunguzi ufanyike na utaongozwa na jaji mstaafu.

Serikali ya Afrika Kusini imesema imesikitishwa na hatua ya Brigety kutoa madai hayo hadharani na sio kufuata utaratibu wa kidiplomasia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor amelizungumzia suala hilo na waziri mwenzake wa Marekani, Antony Blinken.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW