1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini yapata ukakasi kumkamata Putin

Hawa Bihoga
19 Julai 2023

Afrika Kusini ipo njia panda inapojiandaa na mkutano wa BRICS, kama mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ambayo ilitoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladmir Putin wa urusi,italazimika kumkamata .

Afrikanische Delegation zu Besuch in Russland
Picha: Evgeny Biatov/RIA Novosti/picture alliance

Afrika Kusini imesema Rais Vladmir Putin  wa Urusi  hatohudhuria mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi, BRICS, unaofanyika mwezo Agosti, kufuatia makubaliano ya pande mbili, na badala yake Urusi itawakilishwa kwenye mkutano huo utakaofanyika Johannesburg na waziri wake wa mambo ya nje, Sergei Lavrov.

Afrika Kusini ilikabiliwa na hali ngumu katika kuandaa mkutano huo wa kilele kwa sababu, kama mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, ingelaazimika kinadharia kumkamata Putin kwa tuhuma za uhalifu wa kivita endapo angehudhuria mkutano huo.

Mnamo mwezi Machi ICC ilitoa waranti wa kukamatwa kwa Putin, ikimshtumu kwa uhalifu wa kivita kutokana na madai ya ulanguzi wa watoto kutoka Ukraine. Moscow imesema waranti huo hauna uhalali wa kisheria kwa kuwa Urusi siyo mwanachama wa ICC.

Soma pia:ICC yataka Putin akamatwe

Urusi haijaficha mpango ambamo imewahamisha maelfu ya watoto wa Ukraine nchini Urusi, lakini inautaja mpango huo kuwa kampeni ya kiutu ili kuwalinda yatima na watoto waliotelekezwa katika uwanja wa kivita.

Siku ya Jumanne, rais Cyrill Ramaphosa, alisema Moscow ilikuwa imeionya Afrika Kusini kwamba kumkamata Putin itakuwa sawa na kutangaza vita.

Hiyo ilimaanisha kwamba nchi hiyo ilikuwa na matatizo ya wazi na utekelezaji wa ombi la kumkamata na kumkabidhi rais Putin kwa ICC.

Kremlin:Hakuna wakuingilia haki za rais wa Urusi

Hii leo Ikulu ya kremli imesema Urusi haikuiambia Afrika Kusini kwamba kumkata Putin kwa waranti wa ICC itamaanisha vita.

Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Evgeny Biyatov/RIA Novosti/picture alliance

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov,  amewaambia waandishi habari hata hivyo, kwamba kila moja alielewa - bila kulifafanua kwao, ni jaribio la kuingilia haki za Putin linaweza kumaanisha.

"Katika dunia hii, ni wazi kabisaa kwa kila mmoja nini jaribio la kumuingilia mkuu wa taifa la Urusi linamaanisha." Alisema Peskov

 Aliongeza kwamba, hakuna anaehitaji kuelezea kitu chochote.

Afrika Kusini inasemahaiegemei upande katika mzozo wa Ukraine, lakini imekosolewa na mataifa ya magharibi kwa kuonyesha urafiki kwa Urusi, ambayo kihistoria, ni mshirika thabiti wa chama tawala cha Africa National Congress, ANC.

Nchi hiyo imejaribu kuongoza juhudi za upatanishi za Umoja wa Afrika katika mzozo huo, na hapo jana rais wa ukraine Volodymyr zelenskiy, alisema alikuwa na mazungumzo na rais Ramaphosa, ambapo wawili hao waligusia umuhimu wa kuendeleza mpango wa usafirishaji nafaka kutoka Ukraine.

Soma pia:Afrika Kusini yakabiliwa na shinikizo la kisheria kumkamata Putin

Alisema amemualika rais Ramaphosa, kujiunga na mpango wa kiutu wa "Nafaka kutoka Ukraine."

"Sote tuna mtazamo sawa kuhusu umuhimu wa kuendeleza mpango wa nafaka wa bahari nyeusi." Alisema katika hotuba yake.

Afrika Kusini ndiyo mwenyekiti wa sasa wakundi la BRICS, na hapo jana chama chake tawala cha ANC kilikuwa mwenyeji wa vyama washirika kutoka kote duniani:

Katika mazungumzo naibu rais wa nchi hiyo ambaye pia ndiyo naibu rais wa ANC, Paul Mashatile, alizungumzia mzozo unaoendelea kati ya Ukraine na Urusi.

Alisisitiza kuwa Afrika Kusini inaunga mkono kusitishwa kwa mapigano na kupatikana kwa amani ya kweli.

Viongozi wa Afrika wataka kumaliza mzozo wa Ukraine

02:31

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW