1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yaufunga tena mpaka wake na Msumbiji

7 Novemba 2024

Afrika Kusini imeufunga mpaka wake na Msumbiji muda mfupi baada ya kuufungua leo, wakati ambapo ghasia za baada ya uchaguzi katika nchi hiyo jirani yake zikiendelea.

Maandamano mjini Maputo
Maandamano mjini MaputoPicha: Silaide Mutemba/DW

Afrika Kusini imeufunga mpaka wake na Msumbiji muda mfupi baada ya kuufungua leo, wakati ambapo ghasia za baada ya uchaguzi katika nchi hiyo jirani yake zikiendelea na kusababisha makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.

Mamlaka Afrika Kusini pia zimewatahadharisha raia wake waahirishe safari zisizo na umuhimu kuelekea Msumbiji.

Mapema leo, polisi wamewafyatulia mabomu ya kutoa machozimamia ya waandamanaji wa upinzani waliokuwa wanakusanyika katika Mji Mkuu Maputo, kufanya maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi uliopita.

Mashuhuda mmoja aliyezungumza na shirika la habari la Reuters amesema kuwa, walinda usalama walikuwa wamejikusanya katika barabara kuu ya kuingia mjini Maputo, wakati makundi ya watu walipokuwa wanajaribu kuingia mjini humo kwa miguu. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu lililo na makao yake mjini London, Amnesty International limesema kuwa watu 20 wameuwawa na mamia wengine kujeruhiwa na kukamatwa tangu kuanza kwa maandamano hayo mwishoni mwa mwezi Oktoba.