Afrika Kusini yawakamata ndugu wawili kwa ufisadi
7 Juni 2022Atul Gupta na Rajesh Gupta wanadaiwa kuwa mstari wa mbele kwenye mtandao mkubwa wa ufisadi nchini Afrika Kusini chini ya utawala wake Rais wa zamani Jacob Zuma.
Ndugu hao wawili wanatuhumiwa kutumia mahusiano yao na Zuma aliyeongoza Afrika Kusini kati ya mwaka 2009 hadi 2018 kujipatia tenda za serikali, kutumia vibaya mali za umma na hata kushawishi uteuzi wa mawaziri.
Wawili hao ambao walikanusha madai yanayowakabili waliikimbia Afrika Kusini baada ya Zuma kuondolewa maradakani mwaka 2018.
soma pia:Ramaphosa ataka kampuni ya marafiki wa Zuma ichunguzwe
Taarifa za kukamatwa kwa Rajesh Gupta na Atul Gupta zimethibitishwa pia na polisi ya mji wa Dubai ambayo imesema mashauriano yanafanyika kuhusu hatua za kuchukua chini ya makubaliano ya kubadilishana watuhumiwa yaliyotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwaka uliopita.
Kukamatwa kwao kunatazamwa kwa jicho pevu na wachambuzi
Kukamatwa kwao kunajiri wakati umepita mwaka mmoja tangu polisi ya kimataifa Interpol itoe tahadhari ya kuwasaka mwezi Julai mwaka jana.
Wadadisi wa mambo nchini humu wanadai kukamatwa kwao kutaleta hamasa katika uendeshaji wa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili rais mstafu Jacob Zuma.
Dr.Saul Simon wa chuo kikuu cha Stellebosch cha Cape Town. anasema kunaweza kuleta mwelekeo wa tofauti katika kesi inayomkabili Jacob Zuma
" Rajesh ndio alitoa ushahidi kwenye tume ya zondo kwamba alikuwepo wakatu Atul na Ajey walipomshawishi kuanzishwa kwa chanel ya N7" Alisema Dr Saul wa chuo kikuu cha Stellebosch mjini Cape Town.
Kukamatwa kwa ndugu hao wawili katika falme za kiarabu eneo ambalo halikumbatii aina yoyote ya ufisadi, wachambuzi wanasema wamefanikisha hilo ili kulinda hadhi yao kwenye jukwaa la kimataifa.
soma pia:Mzozo wa Zuma na Gupta waigawa Afrika Kusini
Bita Bigenda, mfuatiliaji wa masxuala mbalimbali ya ndani ya Afrika kusini ameiambia DW "muhimu kulinda hadhi yao ili isije kuchukuliwa dubai ni chaka la uhalifu."
Aliongeza kwamba hatua hiyo inaijengea Dubai taswira ambayo ni nzuri katika jukwaa la kimatiafa kwamba si chaka la waovu duniania.
Hata hivyo yamkini mchakato wa kuwaletwa hapa Afrika Kusini ili kesi yao iendeshwe nchini humu ukachelewa lakini majadiliano kati ya mamlaka mbalimbali za kisheria huko Dubai na za hapa Pretoria zinaendelea.