1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yawakamata Wakenya 7 wasikuwa na vibali

17 Desemba 2025

Maafisa wa Afrika Kusini wamewakamata raia saba wa Kenya wanaotuhumiwa kufanya kazi bila kuwa na nyaraka sahihi za ajira.

USA Dulles 2025 | Afrikanische Flüchtlinge aus Südafrika am Dulles International Airport
Afrika Kusini yawakamata Wakenya 7 kwa kufanya kazi bila vibali rasmiPicha: Saul Loeb/AFP

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini imesema Wakenya hao walikuwa wakijihusisha na kazi katika mpango wa serikali ya Marekani wa kuwapokea WaAfrika Kusini Wazungu, au Afrikaner kama wakimbizi.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, uvamizi ulifanyika Jumanne katika kituo cha kushughulikia maombi ya wakimbizi, ambapo raia hao saba wa Kenya walibainika wakifanya kazi huku wakiwa na visa za utalii pekee, jambo linalokiuka wazi masharti yao ya kuingia nchini humo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Wakenya hao walikamatwa na kupewa amri za kufukuzwa nchini, na watapigwa marufuku ya kuingia Afrika Kusini tena kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW