Afrika yakabiliwa na wimbi la 3 la corona
25 Juni 2021Matangazo
Haya yanafanyika wakati ambapo bara hilo likiwa nyuma katika kampeni ya chanjo ya ulimwengu.
Janga la corona limetajwa kuibuka tena kwa kiwango cha kutisha katika nchi zisizopungua 12, huku visa vya maambukizi vikitarajiwa kufikia rekodi ya juu ndani ya wiki tatu.
Mkurugenzi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Afrika CDC, John Nkengasong, ameelezea wimbi la tatu kuwa baya sana.
Hadi kufikia sasa, kirusi cha Delta kilichogunduliwa mara ya kwanza nchini India, kimeripotiwa katika nchi 14 za Afrika.
Idadi kubwa ya maambukizi imeshuhudiwa katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Afrika imeorodhesha maambukizi chini ya milioni 5.3 na vifo ni 139,000.