1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yakumbwa na hofu ya usalama na ukosefu wa ajira

29 Oktoba 2018

Ripoti ya utafiti inaonyesha kuwa kuna hofu ya usalama na ukosefu wa nafasi za ajira katika mataifa ya Afrika

Skyline Dar es Salaam, Tansania
Picha: DW/Eric Boniphace

Utafiti uliotolewa leo unaonyesha kuwa hofu kuhusu hali ya usalama na ukosefu wa nafasi za ajira katika mataifa ya Afrika vinahujumu hatua zilizopigwa katika suala la uongozi katika bara la Afrika katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Ripoti hiyo inaonya kuwa mataifa ambayo yalionekana kuinukia katika uongozi bora yanapoteza dira. Ripoti hiyo inayotolewa kila mwaka na wakfu wa Mo Ibrahim kuhusu uongozi bora barani Afrika pia imesema mazingira ya kibiashara yanazorota na serikali hazina uwezo wa kubuni nafasi za ajira.

Wakfu huo umesema hatua zinapigwa katika mataifa ambayo kuna amani, uwazi wa shughuli za serikali na kuheshimu utawala wa sheria.

Nchi tano zinazoongoza katika utawala bora ni Mauritius, Usheli sheli, Ivory Coast, Namibia na Botswana.

Kenya inatajwa kupiga hatua kwa kusonga nafasi nane mbele kutoka nafasi ya 19 hadi 11, Morocco kutoka nafasi ya 25 hadi 15 na Cote d´Ivoire, imepiga hatua kubwa zaidi kutoka nafasi ya 41 hadi 22. Nchi zinazoshika mkia ni Somalia, Sudan Kusini na Libya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW