1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yatetea viti vya kudumu na kura ya turufu UN

2 Septemba 2024

Nchi za Afrika zinatetea viti vya kudumu na kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Nchi hizo zinasema kuwa jukumu lao muhimu katika juhudi za amani duniani linahitaji uwakilishi mkubwa zaidi.

New York, Marekani | Baraza la Usalama UN
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa katika mikutano yakePicha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Katika mahojiano maalum na DW, Rais wa Malawi Lazarus Chakwera alisisitiza suala ambalo wenzake wengi barani Afrika wamekuwa wakisisitiza kwa miaka mingi: uwakilishi mdogo wa nchi za Afrika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Chakwera amesema wamekuwa wakishinikiza kuangaaziwa upya kwa hali hiyo ili Afrika iwe mshiriki thabiti katika Umoja huo hasa katika Baraza hilo la Usalama na kuongeza kuwa anaibua maswali hayo kila anapopata fursa ya kuzungumza.

Baraza hilo lina wanachama watano wa kudumu: Urusi, Marekani, China, Uingereza, na Ufaransa.

Wote wana uwezo wa kura ya turufu, kumaanisha kila mmoja wao anaweza kupiga kura kivyake kusitisha azimio ili kulinda maslahi yake ya kitaifa, hata kama wanachama wengine wameidhinisha. Viti 10 vilivyobaki si vya kudumu na vimegawanywa kikanda.

Soma pia:Umoja wa Mataifa watoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura ya kibinaadamu

Afrika ina viti vitatu pekee katika baraza hilo lenye wanachama 15, ambavyo kwa sasa vinakaliwa na Sierra Leone, Algeria na Msumbiji. Lakini kwa kuzingatia kuwa mataifa ya Afrika yanajumuisha 28% ya wanachama wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi zimetoa maoni ya kutokuwepo kwa uwakilishi katika mojawapo ya vyombo vya hadhi zaidi vya Umoja wa Mataifa.

Wito wa kupanua Baraza la Usalama umekuwa ukiongezeka hivi karibuni. Sio nchi za Kiafrika pekee zinazotaka uwakilishi zaidi. 

Ingawa kuna hisia jumla kwamba baraza hilo linahitaji kufanyiwa mageuzi, mijadala imekwama juu ya tofauti kuhusu ni kiasi gani cha kupanua baraza hilo, ni nchi gani zitajumuishwa, na ni mamlaka gani linapaswa kuwa nayo.

Afrika haiwezi kusubiri tena

Mnamo Agosti 12, Baraza hilo la Usalama lilifanya mkutano muhimu kushughulikia uwakilishi mdogo wa kihistoria wa Afrika. Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, aliliambia baraza hilo kwamba baada ya miongo kadhaa ya kutafuta sauti kubwa zaidi katika chombo chenye nguvu zaidi cha Umoja wa Mataifa,Afrika haiwezi kusubiri tena.

Bio alisisitiza kuwa Afrika inataka viti viwili vya kudumu katika Baraza hilo la Usalama pamoja na viti viwili zaidi visivyo vya kudumu na kufanya bara hilo kuwa na jumla ya viti vitano visivyo vya kudumu.

Kwanini Umoja wa Mataifa unashindwa kumaliza mizozo duniani?

01:22

This browser does not support the video element.

Bio ameongeza kuwa Umoja wa Afrika utachagua mwanachama huyo wa kudumu na pia kuitaka kura ya turufu kufutiliwa mbali.

Hata hivyo Bio amesema , iwapo wanachama wa Umoja wa Mataifa watataka kura ya turufu kudumishwa, lazima itumike pia na wanachama wote wapya wa kudumu kama suala la haki.

Bio anaongoza kamati ya Umoja wa Afrika ya wakuu 10 wa serikali, inayojulikana kama C-10, ambayo inalenga kuleta mageuzi katika Baraza hilo la Usalama.

Soma pia:Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika zatajwa kuongoza kwa maambukizi mapya ya HIV

Mwaka huu aSerikali za Kiafrika zinataka kutumia mkutano wa COP kupata ufadhili zaidi wa hali ya hewamesikika sana kwasababu Sierre Leone kwa sasa inashikilia urais wa baraza hilo kwa mwezi wa Agosti kama mwanachama asiye wa kudumu katika baraza hilo.

Wakati wa mkutano wa Baraza hilo la Usalama mapema mwezi huu, katibu mkuu wa Umoja wa Ulaya Antonio Guterres, alisema kwamba hawawezi kukubali chombo hicho kikuu cha amani na usalama duniani kukosa sauti ya kudumu kwenye bara lenye zaidi ya watu bilioni na idadi kubwa ya vijana  wanaokuwa kwa haraka,  hii ikiwa ni asilimia 28 ya wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Baraza hilo lililoanzishwa mwaka wa 1945 ili kudumisha amani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, lina uwezo wa kuweka vikwazo, kupeleka ujumbe wa kulinda amani unapohitajika na kupitisha maazimio yanayofunga kisheria. 

Muundo wake unaonyesha muundo wa mamlaka wa baada ya vita wakati sehemu kubwa ya Afrika ilikuwa chini ya ukoloni wa Ulaya.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW