1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afya mbaya ya kiongozi wa kanisa katoliki yawahuzunisha waumini mjini Roma

28 Machi 2005

Vatican City:

Sherehe za pasaka mjini Roma mwaka huu zimegubikwa na hofu kuhusu afya ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Johanna Paulo wa pili.Mbele ya umati wa waumini waliokusanyika katika uwanja wa St Peter,kiongozi huyo wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka 84 alijitahidi awezavyo kuibariki dunia na walimwengu kwa alama za mkono tuu,Urbi et Orbi, bila ya kufanikiwa kutoa kauli.Wengi walitokwa na machozi kumuona kiongozi wao katika hali dhaifu ya afya kama vile.Miaka ya nyuma Papa Johanna Paulo wa pili daima alikua akitoa duwa hiyo kwa lugha zaidi ya 60.Kwa mara ya kwanza tangu Papa Johanna Paulo wa pili akabidhiwe wadhifa huo miaka 26 iliyopita,risala ya pasaka mwaka huu imesomwa kwa niaba yake na msaidizi wake.Katika risala hiyo Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Johanna Paulo wa pili ametoa nasaha amani ipatikane Mashariki ya kati na Afrika pamoja na mafungamano pamoja na maskini wa dunia.