1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afya ya Besigye yadaiwa kudhoofika

20 Januari 2026

Chama cha upinzani cha People's Front for Freedom nchini Uganda kinachoongozwa na Kizza Besigye, kimesema leo kuwa afya ya kiongozi huyo aliyefungwa inadhoofika.

Kizza Besigye katika mahakama ya hakimu mjini Kampala mnamo Mei 25, 2022
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza BesigyePicha: Hajarah Nalwadda/AP/picture alliance

Katika taarifa yake, chama hicho kimesema kuwa Besigye yuko katika hali mbaya kiafya. Aidha, kimetoa wito kwa maafisa wa Uganda kuhakikisha madaktari binafsi pamoja na familia yake wanaonana naye bila vikwazo vyovyote.

Chama hicho kimeendelea kusema ni jambo la kusikitisha kwamba mtu ambaye amejitolea maisha yake kwa afya na uhuru wa wengine ananyimwa haki yake ya kupata utu wa matibabu.

Kwa upande wake, msemaji wa mfumo wa magereza nchini humo Frank Baine, amekanusha taarifa hiyo ya afya ya Besigye na kusema kupelekwa kwake hospitalini kulikuwa kwa ajili ya uchunguzi wa jumla na kwamba leo asubuhi alikuwa akifanya mazoezi yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW