SiasaVatican
Afya ya Papa wa zamani bado ni tete
29 Desemba 2022Matangazo
Tamko hili linatolewa siku moja baada ya makao makuu ya Vatican kufichua kuwa afya ya papa huyo mstaafu Mjerumani mwenye umri wa miaka 95 imedhoofika. Taarifa kutoka kwa msemaji wa Vatican Matteo Bruni imesema Benedict ana fahamu na yuko imara, lakini hali yake haijabadilika tangu jana. Benedict, ambaye katika mwaka wa 2013 alikuwa papa wa kwanza tangu Zama za Kati kujiuzulu kama kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, amekuwa katika hali ya afya iliyodhoofika kwa miaka mingi na hutumia kiti cha walemavu. Kiongozi wa sasa Papa Francis alisema jana kuwa mtangulizi wake huyo ambaye jina lake la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger, ni mgonjwa sana na akawahimiza watu kumuombea.