1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Agosti 15 ni miaka miwili tangu Taliban irejee madarakani

15 Agosti 2023

Kundi la Taliban leo hii linaadhimisha mwaka wa pili, tangu lirejee tena madarakani., Siku kama hii kundi hilo liliudhibiti mji wa Kabul na kuanzisha kile walichokiita usalama wa taifa zima chini ya Mfumo wa Kiislamu.

Afghanistan | Frauen demonstrieren für ihre Rechte
Picha: AFP/Getty Images

Baada ya vikosi vilivyokuwa vikiongozwa na Marekani kutangaza kuondoka katika ardhi ya Afghanistan baada ya miaka 20 ya vita vilivyokuwa havina hitimisho, Agosti 15, 2021 Taliban iliingia katika viunga vya jiji la Kabul, wakati aliyekuwa rais katika kipindi hicho Ashraf Ghani, akiungwa mkono na Marekani akitoroka nchi, na kadhalika vikosi vya usalama vya Afghanistan vilivyoundwa kwa muda mrefu kwa nguvu ya mataifa ya Magharibi vikisambaratika.

Katika taarifa yake msemaji wa mamlaka ya Taliban, Zabihullah Mujahid amesema katika maadhimisho haya ya mara ya pili kwamba mamlaka inatoa pongezi kwa mashujaa wa taifa katika vita hivyo na kuwataka watoe shukrani zao kwa Mungu kwa ushindi huo mkubwa.

Usalama mkali Kabul.

Wanawake wa Afghanistan baada ya kuzungumza na DW mjini KabulPicha: Ali Kaifee/DW

Hali ya usalama kwa siku hii imekuwa kali katika mji mkuu Kabul, askari wakizidisha upekuzi, katika eneo hilo leo Jumanne, ambayo imetangazwa kuwa siku ya mapumziko. Najibullah Ahmadi ni askari anaeongoza doria katika maeneo ya barabara kubwa ambae anasema "Tunamshukuru Mungu hakuna kitisho, hatukabiliwi na vitisho vyovyote, vikosi vyetu vya usalama, Mujaheddin, ujasusi na vingine vyote, mahala popote vilipo kama kutatokea kitisho chochote Mujaheddin wanaweza kukabiliana nacho kwa wakati."

Magwaride ya Talibana yanatarajiwa kufanyika siku nzima na  idara zote, ikiwa ni pamoja na wizara ya elimu, zinafanya mikutano ya kusherehekea. Mujahid anasema hali ya usalama kwa sasa imeimarishwa kwa taifa zima, maeneo yote ya nchi yapo chini ya mfumo mmoja wa uongozi, mfumo wa kiislamu unafanya kazi na kila jambo linatafsiriwa kwa mtazamo wa sharia.

Mawazo ya furaha na wasiwasi katika utawala wa Taliban.

Inaelezwa kuwa raia wa Afghanistan wapo katika kufurahia amani ambayo walishindwa kuishuhudia kwa miongo kadhaa, ingawa Umoja wa Mataifa unasema kumekuwa na matukio kadhaa ya mashambulizi dhidi ya raia, ambayo miongoni mwa hayo yanadaiwa kufanya na kundi hasimu na Taliban, Kundi la Dola la Kiislamu.

Kwa wanawake wengi ambao walifurahia haki zao kwa miongo miwili ya mamlaka iliyokuwa ikiiungwa mkono na mataifa ya Magharibi, hali yao inaripotiwa kuwa mbaya tangu kurejea kwa Taliban.

Katika taarifa yake  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed anasema na hapa namnukuu" Imepita miaka miwili tangu Taliban kuchukua madaraka ya Afghanistan. Miaka miwili ambayo imeyageuza maisha ya wanawake wa Kiafghan na wasichana, katika haki na mustakabali wao.

Soma zaidi:Taliban yaadhimisha miaka miwili tangu kurejea madarakani

Lakini kwa zingatio la hayo yanayosemwa, katika taarifa yake ya sasa msemaji wa mamlaka ya Taliban hakugusua suala lolote lenye utata na hasa kuhusu elimu kwa mwanamke.