Aishi na kifaa cha upasuaji tumboni kwa miaka 18
3 Januari 2017Madaktari nchini Vietnam wameviondoa kifaa cha upasuaji kwa mtu ambae kimekuwemo katika mwili wake pasipo kufahamu kwa miaka 18. Televisheni ya taifa VTV imeripoti kuwa Man Van Nhat, mwenye umria wa miaka 54 amesema kifaa hicho kilisahaulika tumboni mwake mwaka 1998 wakati alipofanyiwa upasuaji wa dharura, uliotokana na ajali ya barabarani. Kwa mara kadhaa Nnat alikuwa akihisi maumivu ya tumbo na alipokwenda hospitali alipewa dawa za kutiliza vidonda vya tumbo. Lakini baada ya uchunguzi wa X-ray, ambao ulifanyika mwaka jana ikabainika kuwa mzizi wa maumivu yake kuwa ni kifaa hicho kilichosahaulika tumboni. Kifaa cha urefu wa sentimita 15 kikiwa kimegawanyika baada ya kumeguka kilikuwa kikimsababishia maumivu bwana huyo. Mkurugenzi wa hospitali ya Back Kan, Trinh Thi Luong, amekiambia kituo cha televisheni cha VTV, kwamba maafisa wapo katika jitihada za kumsaka yule aliyekiacha kifaa hicho katika tumbo la Nhat. Amesema hata kama tayari wamestaafu watawaeleza ili iwe funzo kwa madaktari wengine.