Ajali mbili za ndege zaua watu 19
23 Machi 2009Matangazo
Watu 17 wakiwemo watoto wameuawa kutokana na ajali ya ndege iliyotokea kaskazini mwa jimbo la Montana nchini Marekani.
Msemaji ya idara ya Anga nchini humo amesema kuwa ndege hiyo binafsi ya injini moja ilikuwa ikisafiri kutoka Orville, California na ilianguka baada ya kutua mita 500 kabla ya barabara ya kurukia na kutua katika uwanja wa ndege wa Butte .
Huko nchini Japan, ndege ya mizigo ya kampuni ya FedEx iliyokuwa ikitokea Guangzhou, China imeanguka katika uwanja wa kimataifa wa Nakita jijini Tokyo na kuwaka moto ambapo marubaini wa wili waliyokuwemo wote wamekufa.