1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Ajali ya basi yauwa 14 Ufilipino

6 Desemba 2023

Watu 16 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi nchini Ufilipino.

Ajali ya gari
Ajali ya gariPicha: MARCO SABADIN/AFP

Basi hilo la abiria lililokuwa likitoka katika mkoa wa Iloilo, liliacha njia siku ya Jumanne (Disemba 5) na kuangukia kwenye korongo katika mji wenye milima mingi wa Hamtic katika Jimbo la Antique.

Mtoto mmoja ambaye hakutambulika ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Soma zaidi: Manila yasema meli za China ziligonga kwa makusudi boti za Ufilipino

Mamia ya waokoaji, wakiwemo polisi, askari jeshi na watoa huduma za dharura, walishirikiana kwa masaa kadhaa katika zoezi gumu la kuwaokoa manusura.

Usiku wa Jumanne, mamlaka zilitangaza kusitisha zoezi la uokozi lakini wakawataka raia kutoa taarifa ikiwa maiti zaidi zitapatikana eneo hilo.

Ajali mbaya za gari hutokea mara kwa mara nchini Ufilipino kutokana na kutoheshimu sheria za uendeshaji, magari na barabara mbovu hasa katika maeneo ya milimani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW