Ajali ya boti yawauwa watu 43 kwenye pwani ya Libya
21 Januari 2021Matangazo
Hayo ni kulingana na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia wakimbizi na uhamiaji ambayo pia yamesema wahamiaji wengi 10 wameokolewa.
Mashirika hayo yamearifu kuwa ajali hiyo ya boti ambayo ni kwanza kuripotiwa tangu kuanza mwaka 2021 imefuatia hitilafu ya injini saa chache baada ya chombo hicho kuanza safari yake kutoka mji wa Zawya kuelekea Ulaya.
Manusura wa ajali hiyo ambao ni kutoka mataifa ya Côte d'Ivoire,, Nigeria, Ghana na Gambia wamesema wenzao wote waliokufa pia walikuwa wanatoka mataifa hayo ya magharibi mwa Afrika.
Libya imegeuka lango kuu la safari za wahamiaji kutoka Afrika wanaojaribu kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterrania tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Ghadaffi mwaka 2011.