1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ajali ya helikopta yauwa 18 akiwemo naibu waziri wa Ukraine

18 Januari 2023

Naibu waziri wa mambo ya ndani ni miongoni mwa watu waliokufa baada ya helikopta moja kuanguka katika viunga vya mji mkuu Kiev Jumatano

Ukraine Kiew - Browary | Angriff auf zivile Gebäude | Absturzstelle Hubschrauber mit Innenminister Denys Monastyrskyj
Picha: Daniel Cole/AP Photo/picture alliance

Watu 18 kwa jumla wamefariki kwenye ajali hiyo.Wakati huohuo mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya ameunga mkono hatua ya nchi za Magharibi ya kupeleka vifaru nchini Ukraine.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini  Ukraine Ihor Klymenko ametowa taarifa ya kutokea ajali ya helikopta iliyouwa watu 18 akiwamo naibu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo.

Miongoni mwa waliokufa wamo pia watoto wawili na jumla ya watu 22 wamejeruhiwa wakiwemo watoto 10.Tisa miongoni mwa waliokuwa walikuwamo ndani ya helikopta hiyo ya kutowa huduma za dharura iliyoanguka katika eneo la Brovary,ulioko mashariki mwa mji mkuu Kiev.

Picha: Daniel Cole/AP Photo/picture alliance

Na vyombo vya habari vimeripoti kwamba helikopta hiyo ilianguka karibu na shule ya watoto ya chekechea.Wakati ajali hiyo ikiendelea kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari katika Umoja wa Ulaya nako suala la kupeleka silaha nchii Ukraine linajadiliwa.

Hii leo mwenyekiti wa Umoja huo ameunga mkono suala la nchi za magharibi kupeleka vifaru Ukraine kuisadia nchi hiyo kukabiliana na uvamizi wa vikosi vya Urusi.

Charles Michel rais wa baraza la Umoja wa Ulaya amesema kwa takriban mwaka mmoja Urusi imejielekeza katika mkakati wa kufanya uharibifu,mkakati wa kuendesha ugaidi,ikijaribu kuwashambulia kwa mabomu watu wa Ukraine ili wasalimu amri lakini wananchi wa Ukraine wanapambana.

Picha: John Thys/AFP/Getty Images

Na kwa maana hiyo,amesema wao , Umoja wa Ulaya  wataendelea kuwaunga mkono waukraine kwa namna zote,na kuongeza kusema kwamba wakati ni sasa ambapo Waukraine wanahitaji msaada wa haraka wa vifaa na yeye anaunga mkono hatua ya kupelekwa vifaru vya kijeshi nchini Ukraine.

Upande mwingine Urusi  imeituhumu Marekani  kwamba inaandaa mazingira ya mgogoro ndani ya Ukraine kama sehemu ya kile alichokiita vita vya jumla jamala dhidi ya Moscow.Zelenskyy ahimiza silaha zaidi kwa nchi yake

Tuhuma hizo za Urusi zimetolewa na waziri wake wa mambo ya nje Sergei Lavrov wakati akizungumza  kwenye mkutano na vyombo vya habari huko Moscow.

Lavrov amesema mgogoro wa Ukraine ulianza muda mrefu kabla ya Urusi kupeleka  maelfu ya wanajeshi wake nchini humo mnamo mwezi Februari mwaka jana kutekeleza  kile ilicchokiita operesheni maalum ya kijeshi.Hii leo Marekani nayo imeelezwa kuchukua uamuzi wa kuelekeza nchini Ukraine  silaha zake ilizokuwa imeziweka huko Israel.

Gazeti la NewYorkTimes limechapisha taarifa hiyo leo Jumatano ikisema silaha hizo zinapelekwa Ukraine kuisadia katika mapambano dhidi ya Urusi,na uamuzi huo ulipitishwa mwaka jana.Marekani yawapa mafunzo askari wa Ukraine nchini Ujerumani

Picha: AP

Afisa mmoja wa Israel amelithibitishia shirika la habari la Reuters ripoti hiyo akisema kwamba aliyekuwa waziri mkuu wa Israel wakati huo Yair Lapid aliidhinisha hatua ya kusafirishwa silaha hizo,ingawa Marekani kimsingi haihitaji idhini rasmi kuodowa silaha zake Israel.Kwa miongo wizara ya ulinzi ya Marekani imekuwa ikihifadhi silaha nchini Israel

Marekani na nchi za Magharibi zinaishutumu Urusi kwa kuendesha wanachosema ni mtindo wa kichokozi uliotumiwa wakati wa ukoloni, kuinyakua ardhi ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW