1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUgiriki

Ajali ya treni yazua maandamano Ugiriki

3 Machi 2023

Idadi kubwa ya watu nchini Ugiriki wameingia mitaani kuandamana kupinga hali duni ya miundombuni ya reli baada ya ajali mbaya ya treni iliyosababisha vifo vya takriban watu 57.

Argentinien Krise im Jahr 2001 | Demos
Picha: Walter Astrada/AP Photo/picture alliance

Wafanyakazi wa reli kote nchini humo wamefanya mgomo kwa siku ya pili mfululizo.

 Ajali hiyo mbaya ya treni ilitokea siku ya Jumanne katika mji wa Larissa kati ya treni ya abiria na ile ya mizigo. Shughuli za uokoaji zinatarajiwa kukamilika hii leo.

Maandamano hayo yalianza Alhamisi jioni, wakati maelfu ya watu walipoingia katika mitaa ya Athens na Thesaloniki kupinga hali ya miundombinu ya reli za Ugiriki, ambayo inasemekana kuwa si salama na iliyo katika hali mbaya ya ukarabati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW