1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajira za mda mfupi zinaongezeka Ujerumani

Lillian Urio20 Juni 2005

Utaratibu wa kazi ya nchini Ujerumani unaanza kufanana na ule wa Marekani. Takriban Wajerumani milioni 6.6 wanaopata msaada wa kifedha kutoka serikalini, mwezi wa Machi mwaka huu, walikuwa na ajira za mda mfupi.

Kwa kawaida malipo ya ajira za mda mfupi hazitoshi kuilipia mahitaji yote, kwa hivyo inambidi mtu awe na zaidi ya kazi moja. Takwimu za ofisi ya serikali inayoshughulikia masuala ya ajira nchini Ujerumani, zinaonyesha kwamba mwezi Machi watu takriban milioni 1.7 walikuwa na kazi za pembeni. Na hali hii inazidi kuongezeka.

Bi. Iris Otten wa Munchengladbach anaamka saa kumbi na mbili asubuhi, siku yake ya kazi ya masaa 18 inaanza. Bi. Otten, mwenye umri wa miaka 48 ni mzazi anayelea watoto wake mwenyewe, kwa miaka 9 sasa. Watzoto wake watatu, moja wa kike na wengine wawili wakiume wana umri wa miaka 15, 16 na 19. Kazi zake za nyumbani ni nyingi na hana mda mwingi hadi saa tatu, majira ya mteja wa kwanza kuwasili.

Bi. Otten anapokea wateja katika chumba ambacho hapo awali kilikuwa cha watoto cha kucheza. Sasa hivi Bi. Otten anafanya kazi ya utunzaji wa miguu, inayomletea takriban Euro 150 kila mwezi. Pamoja na fedha hizo, pia anapata fedha kutoka serikalini za kutunza watoto na za kutokuwa na ajira. Lakini hazitoshi.

Euro 1,200 anazozipata kutoka serikalini zinamtosha kwa mahitaji yake muhimu ya kila mwezi. Lakini bado anahitaji fedha kwa ajili ya mafuta ya gari, ili aweze kuwafikia wateja wake wengine. Pia kwa ajili ya nguo na vifaa vya shule vya watoto.

Ndio maana, kwa kipindi cha miaka mitatu, alijifunzwa kuwa daktari wa kutumia dawa za jadi. Na anaifanya kazi hiyo pia, katika chumba anachofanya kazi ya utunzaji wa miguu. Ngugu walimpa mkopo ili aweze kutengeneza hicho chumba. Alishaacha kuwa na matumaini ya kumtegemea Baba wa watoto wake.

Bi. Otten anaeleza:

“Ilivyokuwa mwanzoni ni hivi, walikuwa analipa nusu ya mahitaji yetu, mara nyingine alikuwa analipa, na mara nyingine hakulipa. Ikanibidi niwe natafuta kazi ya aina yoyote ile, ili niweze kulipa nusu yangu. Tangu miaka mitatu sasa hajatoa msaada kabisa na ndio maana ninabidii ili biashara zangu zikuwe”.

Ndio maana anafanya kazi ya kutunza miguu, ana wateja kumi kila mwezi na katika kazi yake ya kuponya kutumia dawa za jadi, bado hana wateja wa kila mara. Faida yake ya biashara anaitumia kwanza kulipa deni la kutengeneza chumba anachofanyia kazi.

Pamoja na kuwashughulikia wateja, Bi.Otten anawalea watoto wake. Kila jioni anatayarisha vifaa kwa ajili ya kazi na wagonjwa wa kesho. Wakati mwingine hadi saa sita za usiku. Lengo lake ni kuacha kutegemea msaada kutoka kwa serikalini.

Frank Herzen kutoka Koln bado hana watoto. Lakini pamoja na hayo anafanya kazi masaa 18 kila siku. Bwana Herzen, mwenye umri wa miaka 33, alikuwa akifanya kazi kama mpishi kwa miaka mingi. Sasa anataka kujiendeleza na amerudi shule kupata elimu ya sekondari.

Somo la kwanza linaanza saa mbili asubuhi. Pia inambidi Bwana Herzen afanye kazi za shule pamoja na kazi nyingine ambazo zinamsaidia kumudu maisha. Ilibidi aache kazi ya upishi kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Ndio maana akaamua kuendelea na elimu iliawe na nafasi nzuri ya kupata kazi nyingine.

Mara mbili kwa wiki baada ya shule, Bwana Herzen anafanya kazi katika duka la kuuza chakula. Walimu wanajua kwamba anafanya kazi na wakati mwingine wanamruhusu atoke darasani mapema asichelewe kazini.

Herzen anaeleza:

“Wakati mwingine ninafanya kazi kwenye baa jioni. Huwa najaribu kutofanya kazi hii siku za katikati ya wiki, lakini wakati mwingine inanibidi. Ikiwa hivyo basi inabidi nikitoka kazini dukani, naenda moja kwa moja kwenye baa. Kazi hii nafanya hadi saa tisa au kumi za asubuhi, na imeshatokea, kwamba baada ya hapo natakiwa kuwa shuleni saa mbili asubuni”.

Mshahara wa kazi ya dukani hautoshi kumudu maisha. Akiuchanganya na mshahara wa kazi ya baa, basi unafikia takriban Euro 1000, kila mwezi. Bwana Herzen hataki kuendelea kuwa na kazi ndogo ndogo nyingini. Kwa mtazamo wake, mtu hawezi kupata ujuzi mzuri kama hana mda wa kukaa kwenye kazi moja kwa mda mrefu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW