Akiba ya chakula yazidi kupungua Haiti
15 Februari 2004Matangazo
PORT AU PRINCE: Nchini Haiti hali ya kusambaza chakula inazidi kuwa mbaya katika maeneo yaliyoathirika na vita vya ndani. Serikali pamoja na mashirika kadha ya misaada zimeonya kuwa chakula kinazidi kuwa haba kwa sababu ya kuzingirwa njia kadha na waasi. Katika maeneo kadha yanayodhibitiwa na waasi akiba ya chakula inaweza ikamalizika baada ya siku nne, ilisemekana. Wafanya biashara kadha waliripoti kwamba waasi wanajaribu kuzuiya uingizaji wa bidhaa za vyakula kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Dominika. - Marekani, Kanada na Jumuiya ya Nchi za Karibik pamoja na Jumuiya ya Nchi za Marekani, OAS, zimemwita Rais Jean Aristide Bertrand na mpinzani wake wautafutie suluhisho la amani mgogoro huo wa ndani nchini Haiti.