Akina Pogba waonesha damu nzito kuliko maji
23 Februari 2017Kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Alhamis iliyopita (16 Februari) katika uwanja wa Old Traford wakati Manchester United na Saint-Etienne zilipokutana, ndugu hao walitafutana tena jana na kubadilishana jezi baada ya mchezo kwenye Stade Geoffery-Guinchard, nyumbani kwa Saint Etienne.
Baada ya kuambiana maneno mawili matatu ilipomalizika mechi hiyo, Paul na Florentin waliongozana kuwatafuta walipo ndugu zao waliokuja kuangalia mechi hiyo, ambapo mama yao, Yeo, na pacha wake Florentin aitwaye Mathias, walikuwa wamevaa jezi zilizoshonwa kwa vitambaa vya timu zote mbili kama walizokuwa wamevaa mjini Manchester. Hata vitambaa vyao vya shingoni pia vilikuwa vya jezi za timu zote.
Uwanjani, Paul aliibuka mshindi baada ya timu yake, Manchester United kuibwaga Etienne kwa 1-0 na hivyo kujiweka kwenye nafasi ya 16 katika Ligi ya Ulaya.
Mwandishi: Mohammed Khelef
Chanzo: Daily Maily UK
Mhariri: Daniel Gakuba