1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Ahly yalazwa bao 1:0 na Al ittihad Kombe la Dunia.

Ramadhan Ali12 Desemba 2005

Al Ahly -mabingwa wa Afrika walazwa na mabingwa wa Asia ,al iitihad katika Kombe la klabu bingwa za dunia.Ethiopia watawazwa tena mabingwa wa Challenge Cup-Kombe la Afrika mashariki na kati huko Kigali.

Baada ya kura ya ijumaa ya Kombe la dunia ijumaa usiku,tiketi 250.000 za Kombe hilo hapo mwakani zinapatikana kuanzia leo katika mtandao wa Internet kupitia utaratibu wa bahati-nasibu-lottery.Maombi ya kununua tiketi hizo yaweza kutolewa kupitia mtandao www.FIFAworldcup.com.Tarehe ya mwisho ya kuuza tiketi hizo kwa mfumo huu ni Januari 15.Bahati nasibu itapigwa Januari 31.

Mshambulizi hatari wa timu ya taifa ya ujerumani wa asili ya Poland-Lukas Podolski anaeichezea Fc Cologne amesema hana uchungu wowote rubidi kuichezea Ujerumani dhidi ya nchi yake ya asilia Poland mjini Dortmund,juni 14.mwakani.

Podolski mwenye umri wa miaka 20 na jogoo wa FC Cologne ni kipenzi wakati huu cha mashabiki wa dimba wa Ujerumani baada ya kutia mabao 10 katika mapambano 17 ya timu ya Taifa .Lukas Podolski alizaliwa katika mji wa Gleitwitz nchini Poland kabla hakuahamia Ujerumani na wazee wake.Podlski alinukuliwa kusema,”mpambano na Poland itakua mechi isiopendeza kwangu,lakini nitacheza kwa juhudi kubwa kuleta ushindi kwa Ujerumani.Itatosha tu ikiwa poland itamaliza nafasi ya pili katika kundi hili linalojumuisha pia Ecuadaor na Costa Rica.” Alisema Podolski.

Ujerumani na Costa Rica ndizo zitakazofungua dimba Juni 9,katika Allianz Arena, mjini Munich,2006.Podolski si mchezaji pekee wa asili ya Poland katika timu ya Taifa ya Ujerumani-kuna 2 wengine:Lukas Sinkiewicz –mlinzi wa Fc Cologne na mshambulizi wa werder Bremen,miroslav Klose.

Ilikua Klose alieufumania jana mara mbili mlango wa FC Cologne na kuipa Bremen ushindi wa mabao 4:1 na kuitosa Cologne tena katika msukosuko wa kuteremshwa chini daraja ya pili.Ulikua mpambano wa 11 FC Cologne imeshindwa kuwika.

Bayern Munich wameshatawazwa magbingwa wa nusu-msimu kufuatia ushindi wao wa 8 hapo jana .Waliizaba Kaiserslauten mabao 2:1.

Bao la kwanza la Munich lilitiwa kwa kichwa na Michael Ballack kabla Muivory Coast, Boubacar Sanogo kusawazisha.Roy Makaay akaipatia Munich bao la penalty kufanya 2:1.kaiserslauten ilipoteza mkwaju wake wa penalty ambao kipa wa Munich, Oliver kahn aliokoa maridadi ajabu.

Hamburg iliendeleza ushindi wake hadi mechi 7 kwa kuikomea Berlin 2:1 na iko sasa nyuma ya mabingwa Bayern Munich huku Bremen ikifuata nafasi ya tatu.Schake iliopo nafasi ya 4 ya ngazi ya Bundesliga ,ilipatwa na msukosuko mwengine baada ya kocha wao Ralf Rangnick kutangaza ataiachamkono mwishoni mwa msimu huu.Schalke ilizaba Manzi 1:0.

Katika Ligi ya Itali, Juventus imepanua mwanya wa hadi point 10 kileleni baada ya kuizaba Calgari jana mabao 4:0.Juventus ina pointi 42 kutoka mapambano 15 ikifuatwa na Fiorentina ilioilaza treviso 1:0.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,Manchester United iliopigwa kumbo nje ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya, ilimudu jana sare tu bao 1:1 na Everton.Manchester United ilipigwa kumbo nje ya champions League na Benefica Lisbon jumatano iliopita.

Katika changamoto za Kombe la dunia la klabu bingwa huko Japan, mabingwa wa Afrika al Ahly ya Misri walivunjiwa jana rekodi yao na mabingwa Asia –al Ittihad kwa bao 1:0.Al Ahly ilikua na rekodi ya kutofungwa mapambano 55,lakini mabingwa hao wa Asia kutoka saudia, waliwaambia wamisri chenye manzo hakaikosi mwisho.Kocha wa al Ahly ,Manuel Jose alilalamika kwamba mabingwa wa Africa hawakucheza uzuri kipindi cha pili.

Mabingwa wa Ulaya,FC liverpool ya Uingereza sawa na mabingwa wa Kombe la Amerika Kusini Libertadores Cup,Sao Paulo ya Brazil zitaingia uwanjani kati ya wiki hii katika hatua ya nusu-finali.Sao paulo itakutana na mabingwa wa Asia Al ittihad mjini Tokyo hapo jumatano.Sydney Fc ya Australia ina miadi na Deportivo Sarissa katika mpambano wapili hii leo.

Mabingwa wa Ulaya Liverpool wamesema wamekwenda Tokyo kujumuisha taji la Kombe la dunia la klabu bingwa na taji lao la mabingwa wa Ulaya.

Katika changamoto ya kanda ya CECAFA:

Ethiopia,imetawazwa mabingwa kwa mara ya pili wa Challenge Cup-kombe la Afrika mashariki na kati mjini Kigali,Ruanda baada ya kuwalaza wenyeji-Ruanda bao 1:0.

Zanzibar Heroes,wamemaliza nafasi ya tatu kwa kuitoa Uganda katika changamoto ya mikwaju ya penalty.hadi firimbi ya mwisho timu hizo mbili zilibakia suluhu 0:0.Kombe lijalo la Challenge Cup litachezwa Uganda mwakani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW