Al-Bashir afikishwa mahakamani mjini Khartoum
21 Julai 2020Omar al-Bashir pamoja anakikabiliwa na mashitaka ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomuingiza madarakni miaka 31 iliyopita. Mahakama nchini Sudan tayari imemhukumu al-Bashir kifungo cha miaka miwili mwezi Desemba kwa mashitaka ya rushwa. Pia anakabiliowa na kesi na uchunguzi kuhusiana na mauaji ya waandamanaji.
Televisheni ya taifa iliripoti ufunguzi wa kesi hiyo katika mahakama mjini Khartoum bila ya kumuonesha al-Bashir, ambaye amefungwa tangu alipoondolewa madarakani Aprili mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi ya utawala wake wa miaka 30.
Soma zaidi: Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir
Al-Bashir amefikishwa mahakamani katika mji mkuu, Khartoum leo kukabiliana na mashitaka ya kwenda kinyume na katiba, kukiuka sheria ya majeshi pamoja na uasi, Al-Moez Hadra, mmoja kati ya kundi la mawakili ambao wamefungua mashitaka ya uhalifu aliliambia shirika la habari la Ujerumani DPA.