1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Al-Shabaab waishambulia hoteli mjini Mogadishu

15 Machi 2024

Wanamgambo wa Al-Shabaab wameishambulia hoteli moja maarufu iliyoko karibu na makazi ya rais mjini Mogadishu jana Alhamisi.

Somalia | Hoteli ya SYL mjini Mogadishu
Vikosi vya usalama vya Somalia vikilinda lango la kuingia kwenye hoteli ya SYL ambayo imeshambuliwa na waasi wenye itikadi kali ya Kiislamu ya al-Shabab, mjini Mogadishu, Somalia.Picha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Duru za kiusalama na mashuhuda wamesema tukio hilo lilitokea kuanzia majira ya saa tatu usiku kwa majira ya nchini Somalia baada ya watu wenye silaha kuivamia hoteli hiyo ya SYL huku wakifyatua risasi.

Haikujulikana mara moja kama kulikuwa na vifo ama majeruhi na baadhi ya mashuhuda walisema polisi walifika muda mfupi baada ya uvamizi huo.

Al-Shabaab wanaofungamana na kundi la kigaidi la al-Qaeda wamekuwa wakifanya uasi dhidi ya serikali ya shirikisho inayotambuliwa kimataifa kwa zaidi ya miaka 16 na mara nyingi wamekuwa wakilenga hoteli ambazo hutembelewa na maafisa wa ngazi za juu wa Somalia na wa kigeni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW