1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Al-Shabaab washambulia kambi ya Umoja wa Afrika, Somalia

27 Mei 2023

Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab, jana Ijumaa, waliivamia kambi ya kijeshi ya Umoja wa Afrika ya Bulo Marer inayotumiwa na wanajeshi wa Uganda nchini Somalia.

Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab wakiwa katika mafunzo ya kijeshi katika viunga vy Mogadishu, Somalia.
Mashambulizi ya makundi ya wanamgambo katika maeneo mbalimbali yamekuwa yakiibua kitisho cha kiusalama. Picha: picture alliance / AP Photo

Shambulizi hilo la wanamgambo wa Al-Shabaab aidha limesababisha kuibuka kwa majibizano ya risasi. Bado haijabainika ikiwa kulikuwa na majeruhi kutokana na mapambano hayo.

Awali, gari lililosheheni mabomu liliendeshwa kuelekea ndani ya kambi hiyo iliyo umbali wa kilometa 120 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu

Kwa mujibu wa Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika linalojulikana kama ATMIS kambi ya Bulo Marer ilianza kushambuliwa na wanamgambo wa Al shabaab saa kumi na moja asubuhi wakitumia  gari hilo lenye vilipuzi na washambuliaji wa kujitoa muhanga.

Akizungumzia shambulio hilo, msemaji wa jeshi la ulinzi la Uganda Felix Kulayigye alithibitisha kutokea kwa shambulio hilo lililowalenga wanajeshi wa Uganda na kuongeza kuwa, jeshi linafanya uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Soma Zaidi:Somalia: Al-Shabaab yakamata kambi ya jeshi ya Janay Abdale

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW