1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Al-Shabaab yashambulia kambi ya jeshi Somalia

18 Januari 2023

Jeshi la Somalia limesema watu wasiopungua 35 wameuawa katika shambulizi la wanamgambo wa al-Shabaab kwenye kambi ya jeshi kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu jana Jumanne.

Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Jeshi la Somalia limesema watu wasiopungua 35 wameuawa katika shambulizi la wanamgambo wa al-Shabaab kwenye kambi ya jeshi kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu jana Jumanne.

Msemaji wa jeshi hilo, Ahmed Mohamed ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA kuwa uvamizi wa al-Shabaab umetanguliwa na miripuko mitatu ya washambuliaji wa kujitoa muhanga.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema liliweza kuidhibiti kwa muda kambi hiyo.

Hata hivyo msemaji wa jeshi amesema hivi sasa kambi hiyo iko mikononi mwa serikali.

Taarifa zimeeleza kuwa waliouawa ni wanajeshi 20 wa serikali pamoja na wanamgambo 15 wa al-Shabaab.

Shambulizi hilo la al-Shabaab limefanyika siku moja baada ya serikali kuukomboa mji muhimu wa mwambao wa Haradhere kutoka mikononi mwa kundi hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW