1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Al-Shabaab yauwa askari 11 wa Somalia mjini Mogadishu

17 Januari 2023

Wanajeshi 11 wa Somalia wameuawa katika shambulizi lililofanywa kwenye kambi yao kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, ambalo kundi la al-Shabaab limedai kuhusika

Somalia Extremistenangriff in Mogadischu
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Kamanda wa kundi la wanamgambo wenye mafungamano na serikali ya mjini Mogadishu, Mohamed Osman ameliambia shirika la habari la AFP kuwa afisa wa cheo cha juu ni miongoni mwa wahanga wa shambulizi hilo, na kuongeza kuwa dazeni kadhaa za wanamgambo wa al-Shabaab wameuawa.

Osman ameeleza kuwa al-Shabaab imeripua gari lililojaa viripuzi kwenye kambi hiyo na kisha wapiganaji wake wakafanya uvamizi. Kamanda wa jeshi la Somalia katika mji wa Balcad ulio karibu na kambi iliyoshambuliwa amesema serikali hivi sasa inalidhibiti eneo hilo.

Shambulizi hilo la al-Shabaab limefanyika siku moja baada ya serikali kuukomboa mji muhimu wa mwambao wa Haradhere kutoka mikononi mwa kundi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW