SiasaSomalia
Al Shabaab yawaua wanajeshi 7 wa Somalia
20 Januari 2023Matangazo
Taarifa ya mashambulizi dhidi ya wanajeshi hao imetolewa na wizara ya habari na kundi hilo la wanamgambo. Afisa mmoja kwenye kambi hiyo ya kijeshi iliyoko kwenye mji wa katikati ya Somalia wa Galcad ameliambia shirika la habari la Reuters, shambulio hilo hatiame lilidhibitiwa.Miongoni mwa waliouwawa ni naibu kamanda wa kambi hiyo ya jeshi aliyekuwa sehemu ya wanajeshi waliopewa mafunzo na Marekani. Shambulio hilo linaonesha kitisho kinachosababishwa na Alshabab kwa wanajeshi wa Somalia, licha ya operesheni iliyoanzishwa na serikali mwaka jana kuonesha ufanisi dhidi ya wanamgambo hao.