1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Al-Sharaa: Raia wa Syria wanapaswa kujiamulia wenyewe

23 Desemba 2024

Mtawala mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa ametoa wito kwa nchi zenye ushawishi katika taifa hilo lililoharibiwa kwa vita kukubaliana juu ya kanuni za jumla kwa ajili ya mustakabali wa Syria.

Syria | Damascus | 2024 | Uturuki | Fidan
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan akutana na kiongozi wa utawala mpya wa Syria, Ahmed al Sharaa, mjini Damascus, Syria.Picha: Murat Gok/Anadolu/picture alliance

Kiongozi huyo wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham HTS baada ya kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema ni muhimu kwa wahusika wakuu wakubaliane juu ya masuala muhimu kuhusu nchi hiyo.

al-Sharaa anayejulikana pia kama Abu Mohammed al-Joulani ameeleza kuwa raia wa Syria wanapaswa kupewa nafasi ya kujiamulia wenyewe juu ya usalama wa nchi yao hasa baada ya mateso yaliyopitia katika utawala uliopita.

Soma pia: Kiongozi mpya Syria aahidi kuheshimu mamlaka ya Lebanon 

Kundi la Hayat Tahrir al-Sham liliunda serikali ya mpito nchini Syria baada ya kuongoza mashambulizi ya waasi yaliyomng'oa madarakani Bashar al-Assad mapema mwezi huu.

Uturuki inachukuliwa kuwa moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa ndani ya Syria, japo Urusi, Iran na Marekani pia zimeonekana kwa kiasi fulani kuwa na ushawishi ndani ya nchi hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW