1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMisri

al-Sisi atahadharisha juu kusambaa vita kwa viwango vya juu

20 Agosti 2024

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ametahadharisha juu ya hatari ya kuenea vita katika Mashariki ya Kati yote kwenye kiwango kisichoweza kudhaniwa.

Misri Cairo | Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Rais Al-Sissi
Rais Abdel Fattah Al-Sissi wa Misri akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, aliyeko nchini humo kuangazia suluhu ya mzozo wa Gaza Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Rais al-Sisi ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaefanya ziara nchini Misri.

Waziri huyo anajaribu kutafuta njia zinazowezekana ili kusonga mbele katika juhudi za kufikia mapatano ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza na kuachiwa kwa mateka wa Israel.

Mazungumzo juu ya kufikia malengo hayo yamepangwa kufanyika baadae mnamo wiki hii wakati ambapo masuala muhimu ya mgogoro huo bado hayajatatuliwa.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW