Viongozi wa Misri na Iraq wakutana kuimarisha mahusiano yao
5 Machi 2023Matangazo
Kulingana na msemaji wa rais wa Misri Ahmed Fahmy, viongozi hao wawili walikutana katika Ikulu ya rais mjini Cairo walikozungumzia ushirikiano wa kiuchumi na Usalama pamoja na masuala ya kikanda ikiwemo ushirikiano wao na nchi jirani ya Jordan.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Mawaziri wa biashara na mawaziri wa masuala ya kigeni wa mataifa yote mawili.
Ziara ya al-Sudan nchini Misri ni ya kwanza tangu bunge lilipoidhinisha baraza lake la mawaziri mwezi Oktoba, hatua iliyomaliza mkwamo wa kisiasa uliodumu kwa mwaka mmoja. Mtangulizi wake Mustafa al-Kadhimi, alianzisha uhusiano wa karibu na Al-Sissi na mfalme Abdulla wa pili wa Jordan.