1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Albania: Maandamano dhidi ya Waziri Mkuu:

22 Februari 2004


TIRANA. Katika mji mkuu wa Albania wafuasi elfu kadha wa upinzani wamefanya maandamano ya kumpinga Waziri Mkuu Fatos Nano. Mkuu wa upinzani Sali Berisha alitoa mwito wa kujiuzulu Fatos Nano na kumfanya dhamana ya ulaji rushwa na mdidimio wa hali za kimaisha wa umma wa Albania. Aliwaita raiya wa Albania wafanye maandamano ya amani. Umati huo uliandamana kutoka uwanja mkuu wa Skanderbeg, kupitia kitovu cha mji mkuu na kumalizia makao makuu ya serikali. Jengo hilo la serikali na taasisi nyingine muhimu zililindwa na polisi zaidi ya 2500. Maandamano hayo yaliitwa na Chama cha Kidemokrasi na makundi mengine yaa upinzani.