1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Albania na utalii wa kimatibabu wa kurekebisha maumbile

7 Novemba 2024

Wakati mmoja, nchi ya Albania ilichukuliwa kama Korea Kaskazini ya Ulaya, nchi iliyotawaliwa na udikteta wa Kikomunisti na iliyojitenga. Lakini sasa imegeuka kuwa kitovu cha utalii wa kimatibabu.

Urekebishaji wa midomo -Botox
Urekebishaji wa midomo -BotoxPicha: Jakub Mrocek/Zoonar/picture alliance

Albania inawavutia mamilioni ya watalii kila mwaka, huku wengi kati ya watalii hao wakienda nchini humo kutafuta kupendezesha tabasamu zao na muenekano mzuri wa midomo yao au pia kwa kina mama kuyatengeneza matiti yao ili yaonekane yakiwa yamesimama hata walio kwenye umri mkubwa ambao kwa kawaida matiti yao huwa yameanguka kutokana na umri au hata kunyonyesha.

Daktari Dritan Gremi, anayeongoza kliniki moja ya urembo katika mji mkuu wa Albania, Tirana anasema hapendi kuzungumzia hali hiyo kama ni utalii wa kimatibabu kwa sababu neno hilo anaona ni kama linatisha kidogo, bali anapendelea kuuzungumzia utalii huo kuwa ni wa furaha, utalii ambao huwafanya watu wafurahi.

Upasuaji wa kubadilisha nyonga Tanzania

03:29

This browser does not support the video element.

Daktari Gremi amesema kliniki yake inatoa huduma za hali ya juu na wanatumia vifaa ambavyo vimehakikiwa na kuthibitishwa kwa viwango vya Ulaya.

Ameeleza kuwa wateja wake wengi ni Wataliano, Wafaransa, raia kutoka Ubelgiji na Uswisi ambao wanavutiwa sana mpango wa matibabu hayo ya urembo unaojumuisha gharama za usafiri na malazi.Waliopona Ukimwi, matumaini ya vita dhidi ya ugonjwa huo

Mamlaka ya afya nchini Albania imesema inatilia maanani na kusisitiza juu ya huduma za hali ya juu. Hii ni kutokana na malalamiko na kashfa za wateja wote wanawake na wanaume waliofanyiwa kazi mbaya katika nchi zingine.

Waendesha mashtaka nchini Albania hivi majuzi walifanya ukaguzi kwenye kliniki zipatazo 30 za vipodozi wakitafuta bidhaa za magendo za kuondoa makunyazi usoni na za kujaza matiti na zile za kutunisha midomo maarufu kama Botox, ambazo zimepigwa marufuku nchini Albania.

 Stephane Pealat amesema alipata kujua kuhusu kliniki ya Gremi wakati alipokwenda kupata ushauri kwa daktari mmoja mwenye asili ya Albania katika mji wa Lyon, Ufaransa.

Urekebishaji wa midomo Picha: picture-alliance/blickwinkel/McPhoto

Baada ya hapo aliitembelea nchi ya Albania mnamo mwezi Agosti na aliweza kuzuru kliniki hiyo katika jiji laTirana, na badae Pealat na ndugu yake waliamua kurudi jijini humo.

Safari ya Stephane Pealat kwenda Albania ilianza kwa matumaini ya kupata tabasamu mpya tena kwa bei nafuu.

Yeye na kaka yake, wanatoka kwenye mji wa Valence wa kusini mwa Ufaransa, na kwa muda mrefu wamekuwa na matatizo ya meno, ikiwa ni pamoja na kupoteza meno jambo ambalo lilimsukuma kutafuta utaratibu mwingine wa upandikizaji wa meno.

Amesema nchini mwao Ufaransa makadirio ya awali ya gharama za huduma ya kupandikiza meno yalikuwa ghali sana na ndipo waipoamua kuanza kuangalia kwenye mitandao kuhusu matibabu ykatika nchi za Bulgaria, Uturuki, Albania na Uhispania.

Kulingana na Pealat, upandikizaji wa meno aliouchagua ungegharimu takriban euro 50,000 nchini Ufaransa, ikilinganishwa na euro 13,500 pekee nchini Albania.

Gharama za chini na kodi nafuu zimezisaidia kliniki za nchini Albania kuwavutia wateja wengi. Sekta ya utalii wa kimatibabu nchini humo inakadiriwa kuingiza kati ya euro milioni 200 hadi euro milioni 250 kwa mwaka.

Hata hivyo Mkuu wa chama cha kitaifa cha madaktari nchini Albania Fatmir Ibrahimaj, amewatahadharisha wagonjwa wa kigeni na wa ndani kuwa wasitegemee sana matangazo ya mitandaoni pekee bali wanapaswa kuhakiki taratibu za urembo kabla ya kufanyiwa matibabu hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi