Algeria kuanzisha mafao ya ukosefu wa ajira kwa vijana
16 Februari 2022Matangazo
Katika mahojiano kwa njia ya Televisheni ya raifa, rais Tebboune amesema malipo hayo yatafanywa kwa lengo la kulinda utu wa vijana.
Malipo hayo ya dinari elfu 13,000 pesa Algeria sawa na dola 92 za Marekani yataanza kutolewa mwezi Machi.
Yataambatana na manufaa ya matibabu, huku kodi kadhaa katika baadhi ya bidhaa za walaji zikiondolewa. Malipo hayo ni sehemu ya bajeti ya mwaka 2022.
Taifa hilo la Afrika Kaskazini linapambana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa karibu asilimia 15. Algeria, ambayo ni muuzaji mkubwa wa gesi barani Afrika na yenye idadi ya watu takriban milioni 45, inaingiza asilimia 90 ya mapato yake kutokana na mafuta na gesi.