1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Algeria yapendekeza miezi sita ya mpito Niger

30 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Ahmed Attaf amependekeza mpango wa miezi sita wa kipindi cha mpito kwa nchi jirani ya Niger.

Niger | General Abdourahmane Tiani
Picha: Balima Boureima/Reuters

Ahmed Attaf ametoa pendekezo lake hilo jana baada ya ziara yake ya wiki iliyopita katika nchi tatu ambazo ni majirani wa Niger. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Algeria ameurudia msimamo wa nchi yake kwamba haitokubali uvamizi wa kijeshi nchini Niger na kwamba haitokubali pia anga yake kutumika na majeshi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS.

Licha ya pendekezo hilo, kiongozi wa mapinduzi wa Niger Abdourahamane Tiani anataka muda wa mpito wa hadi miaka mitatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW