Algiers. Kiongozi wa al-Qaeda auwawa.
27 Aprili 2007Matangazo
Afisa namba mbili wa kundi la kigaidi la al-Qaeda nchini Algeria ameuwawa katika mapigano na kikosi cha jeshi cha doria.
Tangazo hilo lilitolewa na shirika la habari la nchi hiyo la APS na kuwanukuu maafisa wa usalama.
Samir Moussaab aliuwawa karibu na kijiji cha Si Moustapha katika jimbo la Boumerdes, kilometa 40 mashariki ya mji mkuu Algiers.
Mwili wa Moussaab ulitambuliwa na wanachama wa kundi la Salafist la wito na mapambano , ama GSPC, kundi la wapiganaji ambalo lilibadili jina na kujiita al-Qaeda katika Afrika ya kaskazini ya Kiislamu wakati ilipotangaza kuhusika kwake na kundi la kimataifa la al-Qaeda mwezi wa Januari.